fbpx

Raila Odinga – Mwelekeo wa Nchi!

Kiongozi wa NASA Bwana. Raila Odinga (BABA) amekuwa na wakati mkali kuwezesha Kenya Kupata Tume Huru yenye haki na usawa kwa utendakazi wake! Ila! Baada ya Maadai yake kupigiwa chini, hapa chini ni msimamo wa Chama cha NASA (Kwa sasa – Muungano wa Kitaifa wa Mageuzi) kuhusu marudio ya Uchaguzi.Hii ni kupitia waraka wake wa Facebook na Pia Kupitia Chapisho alilolisoma Raila Odinga!

MAAMUZI YA AZIMIO LA UHURU PARK:
1. Muungano wa NASA sasa utajulikana kama Muungano wa Kitaifa wa Mageuzi.
2. Tutaanzisha kampeni za kitaifa za kupinga mamlaka haramu ya serikali na kukaidi mashirika yake.
3. Tutasusia bidhaa na huduma zote za kampuni zinazonufaisha udikteta.
4. Tutabuni KONGAMONO la WANANCHI kuhakikisha utambuaji Katiba na demokrasia.
5. Tutaleta pamoja makundi yote ya utetezi nchini kuhakikisha uchaguzi wa urais unaandaliwa upya kwa njia ya uwazi, haki na usawa katika siku 90.
6. Kuanzia Ijumaa Oktoba 27, hali haitakuwa kawaida. Mambo yatabadilika kabisa.
7. Leo usijihusishe na shughuli ya Jubilee ya kuadaa umma ama kuandaa kura ya maoni, kwa sababu kuna njia nyingi za kumuuwa panya.

Waimbaji wanaendelea kuimba, kutunga nyimbo na Kuandika tanzu za Amani na Ungalifu. Bwana.Raila Odinga, alisema watu wakae makwao na wadumishe amani kwani hii ni vita ya nchi nzima! Unaweza wasilisha ujumbe, maoni,tafiti na vingine kupitia kwa # iliohapa chini kwa mitandao yote ya Kijamii!
#Resist

Click & Call!
%d bloggers like this: